Main Menu

Wednesday, April 24, 2013

BUNGE LA UFARANSA LAIDHINISHA NDOA ZA WATU WA JINSIA MOJA


Bunge la Ufaransa limeidhinisha ndoa za watu wa jinsia moja na kuruhusu wanandoa hao kupata watoto wa kupanga.

Bunge hilo la Ufaransa lenye wabunge wengi wa kisosholisti liliupigia kura mswada huo  kwa kura 331 dhidi ya 225 ili kuidhinisha kuwa sheria.

Sheria hiyo mpya inatarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Baada ya kura hiyo wakereketwa wanaounga mkono ndoa za watu wa jinsia moja walisherehekea uamuzi huo wa bunge na kusema wanastahili kuwa na uhuru wa kufanya maamuzi ya jinsi ya kuendesha maisha yao na kuwa uamuzi huo wa bunge umewapa uhuru huo.

Hata hivyo kumekuwa na upinzani wa kupitishwa kwa sheria hiyo mpya.
 

Punde baada ya kuidhinishwa,wabunge kutoka vyama vya mrengo wa kulia walitangaza kuwa wataupinga kikatiba.

Baraza litakuwa na mwezi mmoja kutoa uamuzi kamili.

Ufaransa ni nchi ya 14 kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja duniani.

0 comments:

Post a Comment