Siku moja baada ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
kuwaarifisha watu wanne ambao amewapendekeza kuongoza wizara muhimu za Fedha, Mambo ya Nje, Habari na Teknolojia ya Mawasiliano na Afya, wananchi wametoa maoni mbalimbali kuwahusu viongozi hao.
Wengi wamefurahishwa na uteuzi wa Balozi Amina Mohammed
ambaye amependekezwa kuongoza wizara ya Mambo ya Nje.
Amina mbali na kuwa mwanamke, pia ni Muislamu na anatoka katika kabila la Kisomali ambalo ni miongoni mwa makabila ya watu wachache.
Hata hivyo baadhi ya Wakenya wametilia shaka uteuzi wa James Wainaina Macharia ambaye amependekezwa kuongoza Wizara ya Afya.
Wanaopinga uteuzi wake wanasema taaluma yake imejikita zaidi katika masuala ya fedha na usimamizi wa Benki na wala sio masuala ya Afya.
Wengine waliopendekezwa ni Henry Rotich (Fedha) na Dkt. Fred Matiangi
(TEKNOHAMA)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment