Maelfu ya wakazi wa mji wa New Delhi
jana waliandamana katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu huo wa India
wakitaka kujiuzulu mkuu wa polisi wa mji huo kufuatia kubakwa na wanaume
wawili mtoto wa kike aliyekuwa na umri wa miaka mitano hivi karibuni.
Wakazi wa New Delhi waliandamana katika mji huo wakishinikiza kujiuzulu
Neeraj Kumar wakati polisi wakimsindikiza mtuhumiwa wa pili mahakamani
hapo jana.
Waandamanaji wamesema wanataka mkuu huyo wa polisi wa New
Delhi ajiuzulu wadhifa huo kwa kuwa ameshindwa kuchukua hatua yoyote ya
kudhamini usalama wa wanawake licha ya kutokea matukio mfululizo
yanayohusiana na usalama wa wanawake kama ya kubakwa.
Wanawake na watoto wadogo pia walikuwa
miongoni wa wakazi wa mji wa New Delhi walioandamana jana kulalamikia
kubakwa binti wa miaka mitano mjini humo.
Hayo yote yanajiri katika hali
ambayo Jumatatu wiki hii mkuu huyo wa polisi ya New Delhi alikataa
kujiuzulu akisema kuwa kujiuzulu kwake hakutasaidia kuhakikisha kuwa
haki inatendeka katika kesi hiyo.
Mtuhumiwa wa pili katika kesi hiyo ya
kumbaka binti huyo wa miaka mitano aliyetajwa kwa jina la Pradeed Kumar
mwenye umri wa miaka 19 alikamatwa juzi katika jimbo la Bihar, ambako
mtuhumiwa wa kwanza Manoj Kumar alitiwa mbaroni pia.
0 comments:
Post a Comment