Main Menu

Sunday, March 3, 2013

WAKENYA WAPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU NCHINI HUMO HII LEO


Serikali ya Kenya imeimarisha usalama kwa kuwapeleka wanausalama laki moja katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Katibu wa kudumu katika Wizara ya Usalama nchini Kenya, Mutea Iringo amesema kuwa, hatua maalumu za kuimarisha usalama zimechukuliwa nchi nzima ili kuhakikisha kuwa, uchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu.

Usalama umeimarishwa kutokana na kuwepo hofu ya kutokea machafuko na tishio la kutekelezwa mashambulio ya kigaidi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Usalama ya Kenya wana usalama hao watakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi huo na kuzuia kutokea vitendo vyovyote vile vya kuhatarisha amani na usalama wa nchi.

Kuna taarifa kwamba, katika baadhi ya maeneo watu wamehama maeneo yao kutokana na hofu ya kutokea machafuko. 



Wakenya leo wameshiriki katika uchaguzi huo huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya uchaguzi, kufuatia machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1,200 waliuawa na wengine zaidi ya laki sita kubaki bila makazi.

Machafuko hayo yalitajwa kuwa makubwa kabisa kuwahi kuikumba Kenya.

Zaidi ya wapiga kura milioni 14 waliojiandikisha kupiga kura nchini Kenya, wameanza kushiriki zoezi la kuchagua viongozi wakuu wa nchi hiyo mapema asubuhi ya leo.

0 comments:

Post a Comment