Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amewaagiza polisi, wakuu wa mikoa na
wa wilaya kutofanya ajizi kwenye suala la wachochezi wa kidini, bali
wachukue hatua stahiki na kwa haraka ili kuendeleza amani ya nchi.
Kikwete alitoboa hayo kupitia hotuba yake ya mwisho wa mwezi aliyoitoa
kwa Taifa kupitia vyombo vya habari .
"Nimewakumbusha polisi na mamlaka husika kote nchini wasifanye ajizi
kwenye matukio ya namna hiyo. Wawachukulie hatua stahiki wale wote
wanaohusika.
Nimewataka wazingatie msemo wa Kiswahili usemao ajizi
nyumba ya njaa," alisema.
Alisema kuwa wachochezi wa mifarakano na chuki za kidini
wasipodhibitiwa ipasavyo wataleta maafa kwa Watanzania wasiokuwa na
hatia akiwataka wakuu wa wilaya na mikoa kutimiza ipasavyo wajibu wao
kama walinzi wa amani.
Alisema wakati wote Serikali haitasita
kuwachukulia hatua wale wote wanaochochea chuki za kidini, wanaodharau
vitabu vitakatifu vya dini nyingine na wanaokejeli dini nyingine.
Kuhusu matokeo mabovu ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012, Rais
Kikwete alitaka utafiti ufanyike ili kujua chanzo na kusisitiza
kwamba bila utafiti wa kina kufanyika , tatizo hilo linaweza kuwa
kubwa na kuligharimu taifa
0 comments:
Post a Comment