Viongozi wa Libya wamesema kuwa, wamewatia mbaroni wahubiri wa Kikristo
wasiopungua 50 kutoka nchini Misri ambao wameingia nchini humo kinyume
cha sheria kwa lengo la kuhubiri mafundisho ya dini ya Kikristo kwa
wakazi wa mji wa Benghazi nchini humo.
Taarifa zinasema kuwa, wahubiri
waliingia nchini humo kwa madai kuwa ni wafanyabiashara, amma makachero
wa Libya waliwatia mbaroni wakati wakitoa mahubiri ya Kikristo kwenye
maeneo ya mji wa Benghazi.
Vyanzo vimeeleza kuwa, jamii ya Libya ni ya
Kiislamu na mahubiri hayo yatasababisha ghasia na machafuko na hatimaye
kupotea uthabiti wa kijamii nchini humo.
radio tehran swahili
0 comments:
Post a Comment