Rais Mwai Kibaki wa Kenya amewataka wananchi wa nchi hiyo kuwa watulivu
kwa minajili ya kuainisha mustakbali wa nchi yao wakati wanapoelekea
kwenye vituo vya kupigia kura na kusisitiza kwamba amani ni msingi wa
maendeleo ya Kenya.
Akizungumza na wananchi kupitia njia ya redio na
televisheni kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika
Jumatatu Machi 4 mwaka huu, Rais Kibaki amewataka wale wote
watakaoshindwa kwenye uchaguzi huo waheshimu matokeo yatakayotangazwa.
Imeelezwa kuwa, karibu watu milioni nne na laki tatu ambao wametimiza
masharti ya kupiga kura wanatajariwa kuelekea kwenye vituo vya kupigia
kura kwa minajili ya kumchagua rais,wawakilishi wa mabunge mawili na
magavana, uchaguzi ambao ni wa kwanza tokea ilipoundwa katiba mpya ya
Kenya iliyobuniwa baada ya kufanyika uchaguzi mkuu mwaka 2007 ambao
uligubikwa na ghasia na machafuko nchini humo.
Uchaguzi wa rais nchini
Kenya una wagombea wanane, ambapo mshindi wa kinyang'anyiro hicho
atapata fursa ya kukalia kiti kinachoachwa wazi na Rais Mwai Kibaki
ambaye amehudumu kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.
radio tehran swahili
0 comments:
Post a Comment