kocha wa real madrid jose mourinho akizungumza na wana habari jijini manchester
Kocha Jose Mourinho amesema dunia
itasimama leo usiku kushuhudia mpambano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real
Madrid na Manchester United.
Kocha huyo wa Real Madrid, anaamini
mchezo huo wa marudiano katika Uwanja wa Old Trafford baina ya timu hizo mbili
bora Ulaya, ungekuwa fainali kwenye Uwanja wa Wembley Mei.
Real, ambayo ilitoa sare ya 1-1
katika mchezo wa kwanza nyumbani Bernabeu wiki mbili zilizopita, lazima ifunge
ili kuweka hai matumaini ya kwenda Robo Fainali.
Mourinho, ambaye anaonekana asiye na
wasiwasi alisema: "Dunia itasimama kuangalia mechi hii. Ina mwonekano wa
fainali, lakini acha tuone timu gani itakwenda Wembley. Nina shaka, matarajio
yanaweza kuwa makubwa,".
kocha wa manchester united sir alex ferguson akifuatilia mazoezi ya timu yake kabla ya mtanange wa leo.
Mpinzani wake, Sir Alex Ferguson
amekubaliana na hilo akisema: "Sitarajii kitu kingine kikubwa katika usiku
huo Ulaya zaidi ya hiki. Klabu kubwa na historia kubwa.
Huu utakuwa mchezo babu kubwa na
sifikirii itakuwa ovyo,".
Real wanajiamini na wako katika hali
nzuri baada ya kuingia Fainali ya Kombe la Mfalme wiki iliyopita kwa kuwafunga
mahasimu wak wakubwa, Barcelona, na pia wakashinda mechi ya ligi dhidi ya
wapinzani wao hao 2-1 Uwanja wa Bernabeu.
Mourinho alisema: "Nani anajua
kitakachotengeneza tofauti katika mchezo - ni maswali dola milioni. Siwezi
kulia ikiwa tutafungwa na nitakimbia mita 100 ikiwa tutashinda.
"Manchester United ni wazuri
kuliko walivyokuwa daima. Tayari wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na ni
Machi tu, hawajafungwa mechi yoyote kwa miezi kadhaa na wametinga Robo Fainali
ya Kombe la FA. Nasi pia tupo katika kiwango kizuri 2013,".
Na kwa matarajio ya Iker Casillas,
ambaye amesafiri na kikosi hicho japo ni majeruhi, Mourinho ana kikosi kamili.
Mourinho alisema: "Wachezaji
wana furaha.
Hatuwezi kushinda ubingwa wa ligi
(La Liga), lakini Ligi ya Mabingwa ni tofauti.
0 comments:
Post a Comment