Main Menu

Tuesday, March 5, 2013

UHURU KENYATA AONGOZA KATIKA MATOKEO YA AWALI NCHINI KENYA

Zoezi la kuhesabu kura katika uchaguzi wa rais nchini Kenya linaendelea, huku matokeo ya awali yakionyesha Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta akiwa mbele ya mpinzani wake, Waziri mkuu Raila Odinga. 

Ikiwa karibu theluthi moja ya kura zimekwisha hesabiwa, Kenyatta alikuwa na asilimia 54 na Odinga asilimia 41, huku wagombea wengine wakiwa mbali mno. 

Hata hivyo, wachambuzi wametahadharisha kuwa maeneo mengi ambayo yamewasilisha matokeo ni yale yanayomuunga mkono Kenyatta. 

Mbali na kumchagua Rais, wapiga kura pia wamewachagua wabunge, maseneta, magavana  na madiwani. Matokeo ya awali yameshatoa washindi katika baadhi ya wilaya, ambapo wagombea kadhaa wamekubali kushindwa. 

Wapiga kura milioni 14.3 walijiandikisha, na mwitikio ulitarajiwa kuvuka asilimia 70 iliyofikiwa mwaka 2007.

0 comments:

Post a Comment