Mkurugenzi msaidizi wa Idara
ya Habari Elimu kwa Umma na Ushirikiano wa Kimataifa Deogratius Egidio ametoa ratiba ya shughuli za kamati
za bunge kabla ya kuanza kwa mkutano wa kumi wa bunge unaotarajiwa kuanza
januari 29 mjini Dodoma.
Egidio amesema mpaka sasa ofisi ya bunge haijapokea
miswada yeyote badala yake kabla ya bunge kuanza wabunge kupitia kamati zao
watakuwa na ziara za kutembelea maeneo mbalimbali hapa nchini.Ametaja baadhi ya maeneo na kamati zitakazotembelea kuwa ni pamoja na kamati ya bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na januari 15 itapokea taarifa ya hali ya ulinzi na usalama kwa kipindi cha julai hadi Desemba 2012 ambapo jumatano watapokea taarifa ya hali ya ushirikiano wa kimataifa na diplomasia duniani hadi kufikia mwezi desemba 2012.
Alhamisi kamati hiyo inatarajia kutembelea gereza la segerea ambapo ijumaa itapokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya APRM Tanzania.
Kamati nyingine ni ile ya Hesabu za serikali ambapo watajadili rasimu ya hesabu zilizokaguliwa za mafungu mbalimbali kuanzia januari 7 hadi 26 na kamati ya miundombinu januari 15 inatarajiwa kupokea taarifa ya utendaji wa shirika la ndege Tanzania ATCL na januari 16 itapokea taarifa ya utendaji wa SUMATRA.
Amesema ratiba zote hizo zinatarajiwa kuanza saa tatu kamili katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es salaam.
Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania
0 comments:
Post a Comment