Main Menu

Sunday, January 13, 2013

WAANDISHI MKOA WA IRINGA WAZINDUA IPC VIKOBA KWA KUCHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 7

 
               mlezi wa ipc na mfanyabiashara maarufu mkoani iringa salum abri akikabidhi cheti pamoja na bahasha yenye shilingi milion mbili ikiwa ni mchango wake kwa ipc vikoba.
 
MLEZI wa klabu  ya  waandishi  wa habari mkoa wa Iringa (IPC) na mfanyabiashara maarufu wa mjini Iringa, Salim Abri (Asas) achangisha  kiasi cha  zaidi ya shilingi milioni 7.4 huku mwenyewe akiwachangia  wanahabari Iringa kiasi cha Milioni 2 taslimu katika harambee ya kuchangia asasi ya kuweka na kukopa ya wanahabari wa mkoa wa Iringa (IPC Vicoba).

Pamoja na Asas pia  mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) amechangia kiasi cha shilingi 500,000 taslimu  wakati mbunge  wa  viti maalum mkoa  wa Iringa Chiku Abwao ( CHADEMA) akichangia  mchango  wa shilingi 150,000 akiwa  wodini anakoendelea  kutibiwa,mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe ameahidi  kuchangia  kiasi cha shilingi 200,000,mbunge wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi akichangia taslim kiasi cha shilingi 100,000
 
 Katika harambee hiyo iliyofanyika  kwenye Mkutano Mkuu wa Wadau wa Habari uliofanyika katika  ukumbi  wa Highlands mjini Iringa blog ya Francis Godwin  iliahidi  kuchangia  kiasi cha shilingi 200,000 Blog ya Mjengwa aliahidi 100,000 wakati mkurugenzi wa Halmashauri ya  Mufindi akichangia  shilingi 300,000 pamoja na benki ya  wananchi Mufindi ambayo pia iliahidi kuchangia  kiasi cha shilingi 300,000.
 
Wengine waliochanga katika harambeee hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu Sh 200,000, Mkuu wa Wilaya Kilolo, Gerald Guninita Sh 200,000 ,na mbunge  wa  viti maalum mkoa wa Iringa (CCM) Rita Kabati (CCM) Sh 100,000.
 
Jeshi la Polisi waliahidi kuchangia Sh 300,000, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma Sh 100,000 Mkurugenzi wa kampuni ya Ujenzi ya GNMS Geofrey Mungai Sh 150,000 na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dk Leticia Warioba Sh 100,000.

Aidha baraza la  vijana la Chadema (BAVICHA) liliahidi  shilingi 100,000,UVCCM Iringa vijijini 100,000,Mwakilishi  wa Habari  leo  Iringa (100,000),IMTV(100,000)Country Fm (100,000),Nuru Fm ( 70,000), Ebony Fm (80,000),Qibla Ten (50,000), Furaha Fm(50,000),ICISO (100,000) madiwani Manispaa ya Iringa (250,000) na wengine wengi.

Wengine akiwemo Mhifadhi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (Tanapa), vyombo vya habari vya mkoani na wadau mbalimbali walichanga kati ya Sh 50,000 na Sh 100,000 huku wanahabari wenyewe wakichanga zaidi ya Sh Milioni 2.
 
 
                                 mtangazaji wa nuru fm abbas (kulia)

Akishukuru kwa michango hiyo, Mwenyekiti wa IPC Vicoba Janeth Matondo aliwashukuru wadau wa habari mkoani hapa kwa kukisaidia chama hicho kupata mtaji.
 
“Mtaji huu utatumika kuboresha shughuli mbalimbali za kimaendeleo za wanahabari mkoani hapa,” alisema.
 
Alisema pamoja na kukopeshwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufanyia kazi, mikopo mingine itakayotolewa italenga kuinua shughuli za kijasiriamali za wanahabari wa mkoa wa Iringa.
 
Awali Salim Abri ambaye pia ni mlezi wa Klabu ya Wanahabari Mkoa wa Iringa (IPC) aliwapongeza wanahabari kwa kuanzisha chama hicho japo amedai kimechelewa kuanzishwa .
 
“Ndugu zangu wadau, wanahabari ni watu muhimu sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa, lakini wengi wao hawajaajiriwa, wanafanya kazi kwa malipo haba, kwahiyo chombo hiki kitasaidia kubadili maisha yao,” alisema na kuwasihi wadau walioahidi kutoa michango kutimiza ahadi zao.
 
Aliutaka uongozi wa IPC kufuatilia michango iliyoahidiwa na kuomba michango zaidi kutoka kwa wadau wengine ili kukiimarisha chombo hicho.

Wakati katibu  mtendaji  wa IPC Frank Leonard amesema  kuwa  lengo la kuanzisha IPC  VIKOBA ni kutaka  wanahabari mkoa  wa Iringa  kujitegemea na kutumia  chombo  hicho  kukopa kwa ajili ya kujenga nyumba ama kununua vitendea kazi .

chanzo fransisgodwin.blogspot

0 comments:

Post a Comment