Mabingwa wa Uganda
timu ya Sports Club Villa imewasili nchini leo mchana tayari kwa ajili ya
mchezo wa kirafiki wa hisani dhidi ya yanga siku ya jumamosi.
Mratibu wa mchezo huo
ambao mapato yake yatasaidia ujenzi wa kituo cha watu wenye ulemavu wa ngozi
Mosi Magere amesema waziri mkuu mizengo panda ndiye atakayekua mgeni rasmi
katika mchezo huo.
Mchezo huo
utatanguliwa na mchezo wa mashabiki wa Manchester United dhidi ya mashabiki wa Yanga.
Timu ya mashabiki wa
manchestar united itaongozwa na Chicharito, Shaffih Dauda, Sebo,Yahaya Mohamedy,
Jeflea, Mbwiga, Kawambwa, na Tupatupa.
Wakati yanga
mashabiki wataongozwa na Maulid Kitenge, Aron Nyanda, Ally mayai, Omary Katanga,
Masudi Kipanya na Ray Kigosi.
Band ya Yamoto itakuwepo
kwa ajili ya kutoa burudani uwanjani hapo.
Makocha wa timu zote
mbili kesho wanatarajiwa kukutana na waandishi wa habari kwa ajili ya
kuzungumzia mchezo huo wa jumamosi.
0 comments:
Post a Comment