Baada ya jana kushuhudia baadhi ya maofisa wa FIFA
wakitiwa nguvuni kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na rushwa katika michuano ya
kombe la dunia, Shrikisho la soka Barani Ulaya UEFA limeitaka FIFA kuhairisha
uchaguzi wa Shirikisho hilo kwa siku ya kesho kutokana na kashfa iliyotokea
hapo jana.
Maafisa saba walikamatwa hapo jana kwa kwa tuhuma za
rushwa na tayari tume huru imeundwa kuchunguza tuhuma zingine za utoaji wa
zabuni za kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ambapo Urusi ndio
muandaaji na fainali za mwaka 2022 za nchini Qatar.
Uchaguzi wa FIFA mwaka huu utawashindanisha Rais
anayetetea kiti chake Joseph Sepp Blatter na Prince Ali Bin Hussein.
Wakati huo huo aliyekuwa makamu wa Rais wa FIFA na Rais
wa CONCACAF Jack Wraner amejisalimisha kwa vyombo vya dola vya nchi yake ya
Trindad na Tobago.
Kuna uwezekano wa Jack Warner akaachiwa kwa dhaman lakini
mpaka hapo Mahakama inayoshughulikia kesi yake itakapoona inafaa.
0 comments:
Post a Comment