Wiki moja baada ya kumalizika kwa
ligi kuu ya Vodacom, timu ya mwadui Fc iliyoapanda ligi kuu kwa msimu ujao wa
2015 na 2016 imeanza kuboresha kikosi chake.
Timu hiyo kutoka mkoani Shinyanga imeanza kwa kukamilisha
usajili wa aliyekua Nahodha wa timu ya Kagera Sugar Maleges Samuel Mwanga kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mwenyekiti wa timu hiyo Joseph Kaasa
amesema kwamba wamejipanga kufanya usajili wa wachezaji zaidi ya 30 ili kuunda
kikosi cha ushindani na ikibidi kutwaa ubingwa msimu ujao.
Kwa upande wake Maleges Samuel Mwanga amewaomba mashabiki wa soka wa timu hiyo kumpa sapoti
kwani anatarajia kufanya mambo mazuri Mwadui Fc .
Maleges alianza soka lake katika timu ya Kagera Sugar ikiwa
daraja la kwanza mwaka 2005 kisha akaenda kucheza soka la kulipwa falme za
kiarabu kabla ya kurejea na kujiunga na timu ya Azam Fc mwaka 2010 alikodumu
kwa mwaka mmoja.
Baada ya hapo alirejea timu ya kagera na kukabidhiwa
unahodha hadi leo alipojiunga na Mwadui Fc.
0 comments:
Post a Comment