Baada ya
kukubali kipigo kutoka kwa watani wao wa jadi, timu ya yanga leo imeingia
kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa kombe la shirikisho dhidi ya
timu ya platinum ya Zimbabwe.
Afisa habari na
mawasiliano wa timu hiyo Jerry Murro amesema tayari waamuzi wa mchezo huo
wameshatajwa ambao watatoka Djibout huku wageni wao wakitarajiwa kuwasili
nchini tarehe 12.
Kambi ya timu hiyo itakua katika hotel ya tasoma na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vitatu vya loyola, karume na taifa.
Katika mchezo wa
hatua ya awali dhidi ya timu ya BDF Eleven ya Botswana klabu hiyo ilizuia mchezo
wake kuoneshwa moja kwa moja, lakini katika mchezo huo wa jumapili uongozi wa
timu hiyo umesema milango ipo wazi kwa chombo cha habari kinachotaka kuonesha
mchezo huo.
Kuhusiana na
kipigo walichokipata kutoka kwa watani wao Simba, Murro anasema kipigo kile
kilitokana na makosa machache ya timu yake na hatafutwi mchawi kutokana na
matokeo yale na hakuna mchezaji yoyote atakayesimamishwa.
Mchezo wa Yanga na
Platinum utafanyika siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa, kabla ya marejeano
wiki mbili baadae nchini Zimbabwe.
Wakati huo huo shirikisho la soka nchini TFF limehairisha michezo miwili ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyokuwa iichezwe kesho (jumatano) kati ya JKT Ruvu dhidi ya Young Africans
katika uwanja wa Taifa, na Mgambo Shooting dhidi ya Azam FC uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga na sasa mechi
hizo zitapangiwa tarehe nyingine.
0 comments:
Post a Comment