Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ameagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa klabu ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini
kuwa mgogoro katika klabu baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka
Kamati ya Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine
kutoka kwa Mwenyekiti huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.
Uamuzi
wa TFF umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba
inayosema: “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba,
kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na FIFA, na kuhakikisha kuwa
zinaheshimiwa na wanachama wake.”
TFF
itatuma wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa
Simba kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya
kusikilizwa.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment