Wananchi wa kata ya Kitwiru wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo
Wakinamama wakifuatilia maelezo kutoka kwa wakufunzi wakujitolea
Mkufunzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu bw john akitoa maelezo kwa wananchi wa kata ya kwa Kilosa manispaa ya Iringa.
Mwangalizi wa haki za binadamu manispaa ya iringa yahaya mohamedy akitoa mafunzo ya katiba na rasimu ya katiba mpya kwa wakazi wa kata ya Nduli manispaa ya Iringa
Mwana mama akiandika maelezo kwa ajili ya matumizi yake ya baadae katika mafunzo hayo
Uchangiaji ulikua wa hali ya juu japo watu wengi hawaijui katiba na rasimu ya katiba
Wakufunzi wakujitolea wa LHRC kutoka kushoto Grace, katikati mwangalizi wa haki za binadamu manispaa ya Iringa Yahaya Mohamedy na kulia ni mkufunzi wa kujitolea bw John.
Wananchi wengi wameonekana kutoijua katiba wala rasimu ya katiba wakati mchakato wa kuipata katiba mpya ukiendelea na sasa ukiwa umefikia hatua ya mabaraza ya katiba ya wilaya kutoa maoni yake.
Wakichangia katika mafunzo ya katiba mpya yanayoendeshwa na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC kupitia wakufunzi wa kujitolea waliohitimu elimu ya juu, wananchi wengi wameonekana kuunga mkono muungano wa serikali tatu.
Wataka baada ya mchakato huu kumalizika uanze mchakato wa kupata katiba ya Tanganyika.
Wengine wamependekeza rais kupunguziwa madaraka ikiwa ni pamoja na kushtakiwa, mapendekezo mengine yaliyotolewa ni pamoja na kuongezwa kwa vipengele vya haki za binadamu ambavyo vitawaangalia wazee, watoto, wanawake, walemavu na makundi mengine maalum.
Aidha wananchi wengine wameitaka tume ya kuratibu maoni ya katiba kuifanyia marekebisho sheria no 8 ya mwaka 2011 inayosimamia upatikanaji wa katiba mpya kwa kua inamapungufu mengi na inaweza kuathiri mchakato mzima.
Kituo cha sheria na haki za binadamu kinatoa elemu ya katiba katika wilaya zote nchini ambapo kwa manispaa ya iringa kimeshafanya katika kata za KITWIRU, NDULI, RUAHA, NA KWA KILOSA, huku kikitarajia kuzifikia kata zilizobaki zikiwemo MTWIVILA, KIHESA, MLANDEGE, MKWAWA, ILALA, MAKORONGONI, MSHINDO, MIVINJENI, KITANZINI NA ISAKALILO,
0 comments:
Post a Comment