KATIKA Kuelekea Redds Miss Ilala
Ijumaa, leo kutakuwa na shindano la kumtafuta mrembo mwenye kipaji (Talent)
itakayofanyika katika mgahawa wa City
Sports and Lounge uliopo katikati ya jiji.
Mratibu wa shindano hilo, Juma Mabakila alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano
hilo yanaendelea vizuri na kueleza kuwa warembo wote 14 wamejipanga kuonesha
vipaji vyao ipasavyo.
Mabakila alisema mshindi wa talent atakabidhiwa zawadi zake kwenye
fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Ijumaa ijayo katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower ulipo
katikati ya jiji.
Mratibu huyo wa Ilala alisema mbali
ya burudani hiyo, pia watatumia nafasi hiyo kuuza ticket za VIP ambazo ni
chache kwa watu maalum, lakini kutakuwa na bahati nasibu itakayotoa pasi za
bure za kusingia katika onesho la Ijumaa.
Alisema kwamba shindano la mwaka huu
litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Ilala maana wamejipanga na
kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa
kupata raha.
“Tumejipanga vizuri kuonesha shoo
nzuri kuanzia hii ya telent na ile kubwa Ijumaa, kutakuwa na vitu tofauti na
ilivyokuwa mwaka jana, kweli mambo yanakwenda vizuri,” alisema Mabakila.
Mashindano ya Redd's Miss Ilala yamedhaminiwa na Redd's
Original,magazeti ya Jambo Leo, Tanzania Daima,Smile, CXC Safaris, Blog ya
wananchi, Fredito na Dodoma wine
0 comments:
Post a Comment