RAIS WA CLUB YA SEVILLA AGOMA KUMUUZA KONDOGBIA.
Rais
wa klabu ya Sevilla Jose Maria del Nido ameviambia vilabu vinavyomuwania kiungo
Geoffrey Kondogbia kuwa nyota huyo
hayupo kwenye mipango ya kuuzwa.
Kondogbia
mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa
akitajwa kutakiwa na vilabu vingi thamani yake imetajwa kufikia Euro milioni 20
kama atahama Sevilla.
Kondogbia
ambaye ni mmoja ya wachezaji waliotwaa taji la vijana na timu ya taifa ya Ufaransa
mwishoni mwa wiki iliyopita aling’ara
kwenye mechi ya kumpongeza nyota
Rio Ferdnand ambapo Sevilla iliifunga Manchester united magoli 3-1.
Vilabu
vya Manchester united , Chelsea, Real Madrid na Juventus vinamtaka kiungo huyo
anayefananishwa uchezaji wake na kiungo wa Manchester City Yaya Toure.
NA MVP Issa maeda wa ebony fm
0 comments:
Post a Comment