Kiongozi wa chama cha MDC nchini Zimbabwe Morgan Tsangirai
ameondoa kesi aliyokuwa amewasilisha mahakamani akiwa na nia
ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais mwezi uliopita yaliyompa
Rais Robert Mugabe ushindi.
Tsangirai ambaye alikuwa waziri mkuu
katika serikali ya mseto pamoja na Mugabe amesema kesi hiyo
iliyopangwa kusikizwa leo haiwezi kuendelea kwasababu tume ya
uchaguzi nchini Zimbabwe bado haijampa nakala alizohitaji kutumia
kuwasilisha hoja zake mahakamani.
Kulingana na tume hiyo Tsangirai
alipata asilimia 34 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi huo huku
Mugabe akitangazwa mshindi kwa asilimia 61.
Katika kesi hiyo
Tsangirai alisema tume hiyo ya uchaguzi ilimpa ushindi Mugabe kwa
njia za udanganyifu ambaye amekuwa akiliongoza taifa hilo tangu
mwaka 1980.
Uchaguzi huo wa mwezi uliopita ulitarajiwa kufikisha
mwisho serikali ya kugawana madaraka kati ya Rais Mugabe na
Tsangirai iliyoundwa mwaka 2008 baada ya uchaguzi uliokuwa na
utata ambao viongozi wa Afrika walikataa kutambua matokeo hayo
yaliyompa ushindi Mugabe ambayo yalikumbwa na hali ya ghasia na
ukandamizaji.
na dwswahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment