Main Menu

Thursday, August 22, 2013

MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA MAWAZIRI WA SEKTA YA MIUNDOMBINU, MAWASILIANO NA HALI YA HEWA WAFANYIKA JIJINI KIGALI RWANDA


Mkutano wa Kumi (10) wa Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Miundombinu, Mawasiliano na Hali ya Hewa unatarajiwa kufanyIka tarehe 23 Agosti, 2013 jijini Kigali. Mkutano huo umetanguliwa na Mkutano wa Wataalamu kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kuanzia tarehe 19-21 Agosti 2013 ambao utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utaofanyika tarehe 22 Agosti, 2013.

Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Miundombinu, Mawasiliano na Hali ya Hewa linategemea kupokea taarifa ya utekelezaji wa Programu na Miradi mbali mbali inayotekelezwa katika nchi Wanachama katika Sekta za Barabara, Reli, Bandari, Hali ya Hewa, Mawasiliano, viwanja wa ndege pamoja na utekelezaji wa maagizo ya Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama ya waliyoyatoa katika Retreat yao ya pili kuhusu ufadhili na maendeleao ya Miundombinu pamoja na maagizo ya Mkutano wa tisa ( 9) cha Baraza la Mawaziri wa Sekta husika wa tarehe 24 Februari, 2012.

 Baada ya kupokea taarifa husika Baraza la mwaziri linategemea kutoa miongozo na maamuzi ya kisera.
Mkurugenzi wa Miundo Mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Ndugu Wambugu 
(kushoto) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu anayehusika na Mindombinu Ndugu Enos Bukuku.
Maafisa Waandamizi kutoa nchi Wanachama wakifuatilia kwa makini Mkutano husika.


0 comments:

Post a Comment