Maafisa nchini Misri wamesema mahakama ya nchi hiyo
imeamuru kuachiwa kwa rais wa zamani Hosni Mubarak.
Mubarak aliitawala Misri kwa muda wa miaka 30 kwa mkono
wa chuma mpaka alipopinduliwa miaka miwili iliyopita.
Hata hivyo ofisi ya waziri Mkuu imesema Mubarak
atawekwa katika mahabusi ya nyumbani,hatua
inayozingatiwa kuwa na lengo la kuwaliwaza wananchi
wengi wa Misri walioshiriki katika maandamano
yaliyomng'oa Mubarak madarakani.
Wachunguzi wanasema kuachiwa huru,kwa Mubarak
kutauchochea zaidi mgogoro wa kisiasa nchini Misri, hasa
baada ya jeshi la nchi hiyo kumwondoa madarakani
Mohamed Mursi.
Mubaraka alihukumiwa kifunguo cha maisha jela mwaka
jana baada ya kupatikana na hatia ya kushindwa kuyazuia
mauaji ya waandamanaji.
NA dwswahili.com
Thursday, August 22, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment