Main Menu

Wednesday, July 10, 2013

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI MKOANI IRINGA WAAGIZWA KUSIMAMIA MATUMIZI YA FEDHA KUTOKA SERIKALI KUU, KATIKA KIKAO CHA RCC MKOA WA IRINGA

 Wajumbe wa kamati ya ushauri ya mkoa wa iringa RCC wakiwa wamesimama kwa dakika moja kumkumbuka mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kilolo Mohamed Gwalima aliyefariki ghafla hivi karibuni, Kutoka kulia mbunge viti maalum Ritta Kabati, Lediana Mng'ong'o, Menrad kigola mbunge wa Mufindi kusini, akifuatiwa mkurugenzi wa halmashauri ya mufindi Bi kalalu.
 Kutoka kushoto mkuu wa wilaya ya kilolo Gerald Guninita, mbunge wa Kilolo Peter Msola na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kilolo.
Mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya mkoa na mkuu wa mkoa wa iringa Dr Christine Ishengoma akifungua kikao hicho, kulia kwake ni mstahiki meya wa manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi na  kushoto ni RAS, Ishengoma amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha kutoka serikali kuu pamoja na kutafuta vyanzo vingine vya mapato.
  Wajumbe wa kamati hiyo kutoka kamati ya ulinzi na usalama
 Kushoto ni mwakilishi kutoka benk kuu ya Tanzania Dr Bernard. Y. Kibesse na mjumbe mwingine
Mkurugenzi wa manispaa ya Iringa Theresia Mahongo akiwasilisha taarifa ya manispaa hiyo 
Meneja wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,Mkoa wa Iringa, Fabian Fundi akiwasilisha taarifa ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka jana na matokeo yake kutangazwa tarehe 30 december mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment