Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti ya www.shaffihdauda.com kutoa maelezo kuhusiana na barua ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake huo.
FIFA
ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya
wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa
barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.
Rais
wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda
alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu,
na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka
nayo.
Wakati
Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala
ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na
viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF
imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya
siku saba.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment