Thursday, April 18, 2013
ZAIDI YA WATOTO MILIONI 22 DUNIANI HAWAJAPATA CHANJO MUHIMU
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema takribani watoto milioni 22 hususan katika nchi zinazoendelea hawajapatiwa chanjo za msingi za kuwakinga na magonjwa hatari.
Katika taarifa iliyotolewa ikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuanza kwa maadhimisho ya wiki ya utoaji chanjo duniani ambayo itakuwa tarehe 20 mwezi huu, WHO inasema mifumo dhaifu ya utoaji huduma za afya pamoja na migogoro ni miongoni mwa sababu zinazowanyima watoto haki ya kupata chanjo za msingi dhidi ya magonjwa kamavile surua, kifaduro, polio, dondakoo na pepopunda.
Shirika hilo linasema ni vyema kuelimisha umma juu ya faida za watoto kupata chanjo na madhara yake iwapo hawatapatiwa.
Mkuu wa kitengo cha chanjo katika Shirika la Afya Duniani Dkt. Jean-Marie Okwo-Bele, anasema chanjo dhidi ya magonjwa hayo huepusha vifo vya watoto milioni tatu kila mwaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment