Main Menu

Thursday, April 18, 2013

ILE CLUB YA KISASA NYANDA ZA JUU KUSINI NA TANZANIA IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO, HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA MUENDELEZO WA UJENZI

Club hii itaitwa LA PARTE jina ambalo asili yake ni nchini hispania.
 Hii ni ngazi kuelekea kaunta ya juu kwa wale ndugu zangu wa VIP
 
        Humu ni choo ambapo kumefungwa vifaa vya kisasa ambapo ukifika tu maji yanatoka na hakuna koki

             Mafundi wakiendelea na kazi upande wa vyoo ambavyo vinafungwa vifaa vya kisasa sana
                           Hapa ndipo itakapokua moja wapo ya kaunta
                               Muonekano muzuri wa club hiyo juu na chini

   Mafundi wakiendelea na kazi katika hatua za mwisho mwsho za upakaji rangi

                                 Hapa itakua kaunta uingiapo tu club
                    Mandhari ya club inavyoonekana wakati ujenzi ukiendelea
               Muonekano kwa nje, kwa wale wakazi wa iringa club hii ipo kando mwa club twisters
       

Kwa mujibu wa meneja wa Ebony Entertainment Ellycoco, Club hiyo itafunguliwa soon pindi ujenzi utakapokamilika kila idara.

Allycoco amesema Club hiyo itakua moja ya Club bora nyanda za juu kusini na Tanzania kwa ujumla kutokana na vifaa na sound ya kisasa itayofungwa ndani ya Club hiyo.

Watu wengi wamekua na shauku na Club hiyo huku wengine wakilalamikia mwenendo wa ujenzi wake kuwa ni wakinyonga.

Club hiyo ipo chini ya kampuni ya BIG TIME ENTERTAINMENT inayomiliki kituo cha radio Ebony Fm kilichopo mkoani Iringa na kampuni ya burudani inayosimamia club  ya TWISTERS na hiyo iliyo katika ujenzi, Ebony Entertainment.

0 comments:

Post a Comment