Main Menu

Tuesday, April 16, 2013

SUMATRA YATHIBITISHA KUONGEZEKA KWA NAULI JIJINI MBEYA

MAMLAKA ya udhibiti usafiri wa Nchi kavu na majini (SUMATRA), mkoa wa Mbeya imetangaza nauli mpya  ya abiria  ambayo imeanza kutumika rasmi kuanzia Aprili 12 mwaka huu, katika Mkoa huo ambapo kwa upande  wa wanafunzi wameanza kulipa nauli ya shilingi mia 2 katika usafiri wa daladala zinazofanya safari zake jijini Mbeya.

Katika taarifa iliyosambazwa na Sumatra katika vyombo vya habari, imesema kwa safari za Mbalizi hadi Mwanjelwa, kadege na Maghorofani imepanda hadi Shilingi 450 kutoka 350, na kutoka Mbalizi kupitia Iwambi, Mwisho wa waya, Ituta(ZZK), Tazara, Iyunga, Nzovwe, Mbembela na Simike  nauli imeongezeka kutoka Shilingi 300 hadi 350.

Aidha taarifa hiyo iliyoainishwa na umbali kwa kilomita inafafanua kuwa abiria wanaotumia njia ya Stendi Kuu/Mbalizi, Mwisho wa waya na Iwambi nao wanalipia Shilingi 450 badala ya shilingi 350 ambapo katika vituo vya Sokomatola, rufaa, City (Mbeya Recto), Azimio, mabatini, Meta, Simike, Mbembela, Nzovwe, Iyunga na Tazara wanalipia Shilingi 400 badala ya 300 ya awali.

Ofisa wa Sumatra mkoa wa Mbeya, Amani Shamaje amethibitisha nauli hiyo kuongeza kwa safari za Stendi kuu hadi Igawilo na uyole kati imefikia Shilingi 500 kwa mtu mzima badala ya Shilingi 400 ya zamani ambapo Stendi kuu hadi Jeshini (JKT), Kilimo na uyole ni shilingi 400 kutoka shilingi 350 ya awali.

Amesema  katika vituo vingine vya katikati kutoka Stendi kuelekea uyole ambavyo ni Sokomatola, Rufaa, BP, Benki, Sinde, Stereo, Fine, Mwanjelwa, Soweto, mama John, CCM, Ilomba, Sai na RRM nauli imefikia Shilingi 400 kutoka Shilingi
300.

0 comments:

Post a Comment