Katika uchaguzi wa urais nchini Venezuela,
Nicolas Maduro, mrithi wa aliyekuwa rais wa
taifa hilo, Hugo Chevez, ameshinda kwa
kupata asilimia 51 ya kura.
Huo ulikuwa
uchaguzi wa kwanza kufanyika nchini humo
tokea kufariki kwa kiongozi wa kisoshalisti,
Hugo Chavez.
Hata hivyo mshindani wake,
kiongozi wa upinzani Henrique Capriles,
ambaye pia ni Gavana wa jimbo la Miranda,
alijijenga katika umaarufu mnamo siku za
karibu hadi kufikia asilimia 7 nyuma ya
Maduro.
Kiongozi huyo wa upinzani, Henriuqe,
aliyeshindwa na hayati Chavez katika
uchaguzi wa mwaka jana, amelalamika juu ya
uchaguzi huo.
Amemlaumu Rais wa sasa
Maduro kwa kuyatumia vibaya mamlaka ya
serikali na kwa kukiuka sheria za uchaguzi.
Kwa upande wake Maduro alidai kwamba
kambi ya mrengo wa kulia iliendesha
kampeni chafu dhidi yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment