Kamati ya Utendaji ya Chama Cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kwa mamlaka iliyonayo imeteua kamati mbali
mbali zitakazoshirikiana na Kamati ya Utendaji katika kukabiliana na changamoto
mbali mbali za mpira wa miguu katika Mkoa wake ili kuweza kufikia malengo yake
waliyojiwekea. Wafuatao
ni watu na kamati mbali mbali walioteuliwa/zilizoteuliwa na Kamati ya Utendaji
ya Chama Cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam:
Bw. Joseph Kanakamfumo Mkurugenzi wa Ufundi
Bw. Saidi Pambalelo Afisa Tawala
Bw. Mohamedi Muharizo Afisa Habari
Bw. Hashim Abdallah Afisa Usalama
KAMATI YA FEDHA NA
MIPANGO
1. Bw. Meba Ramadhani
Mwenyekiti
2. Bw. Iddi Msonga Makamu Mwenyekiti
3. Bw. Ali Hassani
4. Bw. Ramadhani Kilemile
5. Bw. Isack Mazwile
KAMATI YA UFUNDI NA MASHINDANO
1. Bw. Kenny Mwaisabula Mwenyekiti
2. Bw. Shabani Mohamedi Makamu Mwenyekiti
3. Bw. Hugo Seseme
4. Bw. Daudi Kanuti
5. Bw. Kassim Mustapha
6. Bw. Abeid Mziba
7. Bw. Bakari Mtumwa
KAMATI YA MAENDELEO YA SOKA
LA VIJANA NA WANAWAKE
1. Bw. Benny Kisaka Mwenyekiti
2. Bw. Muhsin Balhabou Makamu
Mwenyekiti
3. Dr. Sesy Makafu
4. Bw. Emmanuel Kazimoto
5. Dr. Maneno
Tamba
6. Bw. Edwin Mloka
7. Bw. Sande Mwanahewa
8. Bw. Richard Shayo
KAMATI YA WAAMUZI
1. Bw. Jovin Ndimbo Mwenyekiti
2. Bw. Sijali Mzeru Makamu
Mwenyekiti
3. Bw. Saidi Mbwana
4. Bw. Benny Mtula
5. Bw. Abdallah Mitole
KAMATI YA NIDHAMU NA
USULUHISHI
1. Mheshimiwa Roman Masumbuko Mwenyekiti
2. Bw. Fahadi Faraji Kayuga Makamu
Mwenyekiti
3. Bw. Mohamedi Mpili
4. Bw. Peter Nkwera
5. Bw. Jimmy Mhango
KAMATI YA RUFAA
1. Mheshimiwa Salehe Njaa Mwenyekiti
2. Bw. Saidi Engo Makamu Mwenyekiti
3. Bw. Abasi Kuka
4. Bw. Yusuph Macho
5. Bw. Boi Risasi
Pia Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam inapenda kuwafahamisha wanachama wake, wadau na mashabiki
wa mpira wa miguu Tanzania dhamira yao ya kuendeleza mpira wa miguu katika Mkoa
wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Kwa kuanzia Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam kipo kwenye mchakato wa kukamilisha DRFA
Strategic Plan 2013 - 2016 (Mpango Mkakati Kazi) kwa kipindi cha miaka
minne pamoja na kuboresha Financial
Regulations zake ili kiweze kuwa na dira ya kuwahudumia wadau wake kwa ufanisi
na uwazi zaidi. Lakini pia Kamati ya Utendaji imeona haja ya Chama Cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na Website
yake kwa ajili ya kuwapa habari wadau wake na Watanzania kwa ujumla.
Mwisho Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kinaomba ushirikiano na wadau wote wa mpira
hususani Serikali, TFF, Vyama vya Mikoa, Walimu, Waamuzi, Madaktari, Vilabu,
Makampuni na Waandishi wa habari na Vyombo vya habari katika kuendeleza mpira
wa miguu katika mkoa wa Dar es Salaam na hatimaye mikoa yote ya Tanzania. “Kwani Pamoja Tunaweza”
Ahsanteni,
Almasi
Kasongo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA)
0 comments:
Post a Comment