Main Menu

Monday, January 7, 2013

WAHAMIAJI HARAMU WAFA KATIKA AJALI NCHINI ANGOLA



Lori lililokuwa limebeba wahamiaji haramu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limepata ajali na kuua wahamiaji 16 kati yao, huku wengine wakijeruhiwa vibaya. 

Wahamiaji hao haramu walikuwa wakisafiri kutoka katika eneo la mpakani la Soyo la kaskazini magharibi mwa Angola kuelekea mji mkuu Luanda. 

Kamanda wa Polisi wa eneo lilipotokea ajali Bwana Andre Massota amesema kuwa, wahamiaji hao haramu walikuwa wamefichwa katika kontena la lori hilo; na wengi wao walifariki dunia baada ya kuminyana na kukosa pumzi. Ameongeza kuwa, iliwachukua polisi masaa mawili kufanikiwa kufungua kontena hilo. 

Dereva wa Lori hilo aliyechukua ujira wa dola 200 za Kimarekani ili kuwavusha wahamiaji hao mpaka Luanda alitoweka mara tu baada ya kutokea ajali. 

Itakumbukwa kuwa, katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, zaidi ya wahamiaji 30 wengi wao wakiwa ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walirejeshwa katika mpaka wa nchi hiyo kutoka Angola.

RADIO TEHRANI

0 comments:

Post a Comment