Moja kati ya stori zinazomiliki
headlines sasa hivi Nigeria ni hii ya wachungaji wawili mashoga
kushitakiwa kwa kosa la kumlazimisha mwanaume mwenzao kufanya nao hayo
mapenzi ya jinsia moja.
Wachungaji wenyewe ni Prince Ejimole (26) na Lawrence Udo (25) ambao walikamatwa na polisi wakiwa kwenye chumba cha hoteli.
Isue ilibuma pale muumini wao mmoja alipoomba msaada wa kufanyiwa maombezi ambapo
wachungaji hao walimualika kwenye chumba cha hoteli ambayo siku zote
ndio wamekua wakifanya hayo mambo yao kwa siri.
Muumini aitwae Chidiebere ambae
ni mwanaume alipofika chumbani hotelini badala ya kuanza kuombewa
akajikuta akipapaswa kimahaba na mmoja kati ya wachungaji hao ambae
alianza kumvua nguo mpaka kumshika kwenye sehemu zake za siri.
Chidi alipoona hivyo akapiga
kelele na kuita uongozi wa hoteli ambao nao waliwaita polisi waliokuja
kuwakamata wachungaji hao, wahudumu wa hoteli hiyo hawakua wameushtukia
mchezo kwa sababu siku zote wachungaji hao wanapokuja kukodi chumba
wanajua wamekuja kwa ajili ya maombi manake hata kelele za maombezi huwa
wanazipiga.
Kesi yao tayari iko Mahakamani na imesomwa leo january 7 2013.
Monday, January 7, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment