Main Menu

Monday, January 7, 2013

MADAKTARI MSUMBIJI WAANZA MGOMO WA SIKU TANO LEO



Madaktari nchini Msumbiji leo wameanza mgomo wao wa siku tano wakidai nyongeza ya mishahara na kuboreshwa mazingira yao ya kazi. 

vyanzo vya habari mjini Maputo, vimeinukuu Jumuiya ya Madaktari nchini Msumbiji ikitangaza kwamba, kuanzia leo madakatari wote wanagoma kufanya kazi kwa muda wa siku tano ili kuishinikiza serikali ya nchi hiyo isikilize matakwa yao ya nyongeza ya mishahara pamoja na kuboreshwa mazingira ya kazi na makazi.

Hata hivyo jumuiya hiyo imesema kuwa, kitengo cha huduma za dharura kitaendelea na shughuli zake kama kawaida. Madaktari hao wanadai kwamba, kwa kiwango cha chini wapatiwe mshahara wa Metical elfu tisa ambazo ni sawa na Euro elfu mbili kwa mwezi. 

Hii ni katika hali ambayo serikali imependekeza mshahara wa Metical elfu 3 hadi elfu ambazo kwa mwezi ni chini ya Euro elfu moja. Katika radiamali yake ya mgomo huo wa madakatari, Wizara ya Afya ya Msumbiji imetangaza kuwa, haitaruhusu mgomo huo uwahusishe wafanyakazi wa vitengo nyeti vya wizara hiyo.

kwa niaba ya vyombo vya habari vya kimataifa.

0 comments:

Post a Comment