naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia january makamba
Masaa machache kabla ya kuhamia rasmi katika mfumo wa urushaji matangazo ya televisheni wa digital,
Serikali imesua sua na kuamua zoezi hilo kufanyika katika mkoa mmoja tu katika awamu ya
kwanza.
Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam, Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba, amesema serikali imehairisha zoezi hilo kwenye mikoa iliyotajwa hapo awali kutokana na baadhi ya mikoa hiyo kutofikiwa na teknolojia hiyo kwa wakati.
Makamba amesema serikali kwa kushirikiana na mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA wamekubaliana kufanya zoezi hilo kwa mkoa wa dar es salaam pekee katika awamu ya kwanza na mkoa mingine katika awamu nyingine.

aidha kuhusiana na malalamiko yanayotolewa na wananchi kuhusu upatikanaji wa ving’amuzi na huduma zinazotolewa, Makamba ameyataka makampuni yaliyopewa leseni kuweka utaratibu wa kuwasikiliza wananchi na kuboresha matangazo hayo.
0 comments:
Post a Comment