Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya Mamlaka ya mawasiliano
Tanzania TCRA kusimamisha rasmi urushwaji wa matangazo ya analojia kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania inaamini kuwa huduma ya M-Pesa itabakia kuwa
njia salama zaidi na ya kipekee itakayo wawezesha Watanzania popote walipo
kulipia vifurushi vya vingamuzi vyao kwa urahisi na usalama zaidi.
Mkurugenzi mtendaji
wa Vodacom Tanzania Rene Meza amesema kuwa anaamini urushwaji wa matangazo kwa
njia ya digitali ni hatua moja ya maendeleo kwa taifa na kwamba Watanzania
wasiwe na hofu ya sumbufu wa kupanga foleni ili kulipia huduma za televisheni
kwa kuwa kila mmoja anaweza kufanya hivyo kutoka kiganja cha mkono wake kwa
urahisi na haraka kupitia M-pesa wakati wowote na mahali popote.
“Dunia ya sasa inatumia
kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Sayansi na
teknolojia ili kurahisisha maisha ya watu wanaoishi humo, nasi tunapaswa
kuhakikisha tunaendana na mabadiliko hayo, Vodacom itaendelea kuwa kiungo cha
mbadiliko ya maisha ya ya watanzania kupitai teknolojia za simu.” alisema Meza
na kuongeza kuwa, “Katika mchakato huu wa kuhamia digitali kutoka anolojia
huduma yetu ya M-pesa itasimama kuwa kiungo muhimu cha kuwaondolea wananchi
kero ya kulipia huduma kila mwishoni mwa mwezi.
Meza aliongeza kuwa
ni vyema sasa Watanzania wakatumia huduma ya M – Pesa kufanya malipo ya
ving’amuzi vyao ili kuokoa muda na usumbufu ambao wanaweza kuupata kutokana na
msongamano wa watu katika maeneo ya maouzo kwani ndio njia pekee rahisi na
salama ambayo tayari imewawezesha wateja wake kufanya malipo hayo.
“Tunaamini katika
kutoa suluhisho la kibiashara kwa wateja wetu, kwa wateja wenye ving’amuzi
wanaohitaji kununua vifurushi kwa njia ya M-Pesa wanapaswa kupiga *150*00# na
kisha kuchagua namba 4 Malipo, na kisha
kuchagua 1 na kuweka namba ya kampuni na kuweka namba ya kumbukumbu ambayo iko
katika king’amuzi chake, na kisha atachagua aina ya malipo anayotaka kufanya na
kuingiza namba yake ya siri na kubonyeza 1 kuthibitisha,” alisema Meza.
Mpaka sasa mamlaka ya
mawasiliano Tanzania imetoa vibali kwa kampuni zenye mamlaka ya kurusha
matangazo kwa mfumo wa dijitali ambapo Star Media, Agape Assosiate Limited
ambazo tayari zimekwisha ingia katika ushirikiano na kampuni ya Vodacom
Tanzania kuwawezesha wateja wake kufanya malipo kupitia huduma ya M-Pesa.
0 comments:
Post a Comment