Main Menu

Thursday, July 2, 2015

HIVI NI VITU VINAVYOMFANYA RONALDO AHESHIMIKE ZAIDI NJE YA UWANJA, FUATILIA KISA HIKI



Miracle tsunami survivor Martunis, who was missing for 21 days after 2004 disaster, signsDunia tunayoishi ina mambo mengi sana, yapo mambo ya kufurahisha na mengine ya kusikitisha na kuhuzunisha.

Ipo mikasa mingi ya kimaisha ambayo huwakumba wanamichezo na hata wale ambao wanandoto ya kuwa wanamichezo wakubwa hapo baadae.

Embu fuatilia stori ya kijana Martunis aliyenusurika na tetemeko la ardhi na sasa anategemea kuwa na ndoto za kuwa mchezaji mkubwa duniani hapo baadae.
Martunis ni kijana ambaye amezaliwa na kukulia katika eneo linalojulikana kama  Banda Aceh nchi ya Indonessia.

Mwaka 2004 kulitokea tetemeko kubwa sana  lijulikanalo kama Tsunami katika ukanda wa bahari ya Indi na kuua watu takribani laki 230,000 katika nchi za ukanda wa bahari ya Indi ikiwepo Singapore.

Temeko hilo lilibadili sura na maisha ya Muritius kutokana na kumpoteza mama yake na kaka zake wawili.

Katika tetemeko hilo,Martunis  naye alizolewa na maji na kusukumwa hadi beach na kujikuta amekaa kwenye dimbwi la maji karibu na bahari. 
 Martunis has now signed with Sporting's academy and posed for photos at the Estadio Jose Alvalade
Alikaa hapo kwa muda wa siku 21 akila vyakula vilivyosombwa na maji kuletwa hapo alipo baada ya Tsunami kutokea.

Mauritius alikutwa hapo na kikundi cha waandishi wa Habari akiwa anashangaa ufukwe wa mji wa Indonesia   akiwa amevaa jezi namba 10 ya mchezaji wa Ureno Rui Costa ambayo alikua amevaa wakati anasombwa na maji.
 
Alipelekwa hospitali na kutundikiwa dripu kwa sababu uchunguzi wa kitabibu ulionesha kuwa Martunis alikumbwa na ugonjwa wa ….Mmoja kati ya wanachama wa kikundi cha kuokoa watoto alisema kuwa endapo wangechelwa kumokoa kwa siku moja,basi Martunis angekutwa amekufa.

Alivyoulizwa kuhusu jinsi alivyonusurika kifo Martunis alisema kwamba “Nilikua siogopi kwa wakati ule kwasababu bado nilikua nataka kuendelea kuishi na kuwaona ndugu zangu na pia kuwa mcheza mpira”
 Real Madrid star Cristiano Ronaldo was inspired by Martunis' story and met with him after the disaster
Story yake iligusa nyoyo za watu wengi akiwemo mchezaji wa Portugal Cristiano Ronaldo, Ronaldo  baada ya kujionea hali ya Muritius, alijitolea kwa kumlipia ujenzi  wa nyumba yao mpya  ambayo iliharibiwa na Tsunami. 

Martunis ameshakutana na Cristiano Ronaldo mara nyingi na hivi karibuni alikutana nae mwaka 2013. 

Mwaka 2005 Martunis alikutana na kikosi cha Ureno akiwemo shujaa wake CR7 na akasema siku moja angependa kuchezea timu ya taifa ya Ureno.

Habari nzuri kwa sasa ni kwamba Martunis atacheza timu ya under 19 akiwa na club ya Sporting Lisbon ambapo Cristiano Ronaldo alipitia. 
 The late Portuguese legend Eusebio is pictured with the youngster in a new Portugal shirt in 2005
Lisbon imesajili mchezaji huyo ambae toka kitambo alikua na ndoto za kucheza soka ili awe kama nyota wa Ureno ambao ni Cristiano Ronaldo na Luis Figo.
 Along with Ronaldo, Portuguese icon Luis Figo is one of the Sporting academy's most famous products
Kituo cha vijana cha soka cha Sporting Lisborn kimewatoa nyota wengi sana katika mchezo wa soka, Miongoni mwa nyota hao ni pamoja na Cristiano Ronaldo, Luis Figo, Luis Nani, Erik Dier, Ricardo Quaresma, Simao, Joao Moutinho, Jose Fonte, Nuno Valente, Silvestre Valera, Miguel Velso na Luis Boa Morte.

Akizngumzia juu ya usajili wa chipukizi Muritius,Rais wa klabu ya Sporting Lisbon Bruno  De Carvalho anasema” Martunis atafanya kazi katika kituo cha vijana cha Sporting Lisbon.

Tutafanya kazi naye na kumuendeleza ili jae kuwa mtu mzuri katika na mchezaji mkubwa katika klabu ya Sporting.

Kwa upande wake Martunis anasema kuwa” kucheza klabu ya Sporting Lisbon ni ndoto ambayo imetimia.”

Kila la kheri Martunis katika maisha yako mapya kunako klabu ya Sporting Lisbon.

0 comments:

Post a Comment