Main Menu

Saturday, July 4, 2015

ARGENTINA, CHILE FAINAL YA KUFA MTU, JIFUNZE KITU KUPITIA MAKALA HII



The Barcelona forward trains alongside his Argentina team-mates ahead of the match against ChileMichuano ya Copa Amerika itafikia tamati leo kwa mchezo wa fainali kati ya wenyeji wa michuano hiyo timu ya taifa ya Chile na timu ya taifa ya Argentina.Hakika hili ni bonge la fainali.

Hii itakuwa fainali ya tano kwa timu ya taifa ya Chile katika michuano ya kombe la Amerika ya kusini kwani tayari Chile wamekwishacheza fainali nne za michuano hiyo.

Timu ya taifa ya Chile ina rekodi ya kucheza fainali nne za michuano ya Amerika Kusini pasipokutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Fainali walizocheza  Chile katika michuano ya Copa Amerika ni mwaka 1955 walipofungwa na timu ya taifa ya Argentina goli moja kwa sifuri goli lililofungwa na na Rodolfo Micheli dakika ya 59.

Fainali nyingine walizocheza Chile ni za mwaka 1956 wakifungwa na Uruguay,mwaka 1979 wakifungwa na timu ya taifa ya Paraguay  na mwaka 1987 wakifungwa na timu ya taifa ya Uruguay goli moja kwa sifuri goli la Pablo Bengoechea katika dakika ya 56.

Endapo Chile watachukua ubingwa wa Copa Amerika mwaka huu,utakuwa ubingwa wao wa kwanza wa michuano hiyo.

Vipi kwa wapinzani wao timu ya taifa ya Argentina?Kwa Argentina hii ni fainali yao ya  27 ya michuano ya Copa Amerika huku wakichukua mara 14 na mara 12 wakiwa washindi wa pili.
Arsenal forward Alexis Sanchez is the main threat for the host nation against the favourites
Mara ya mwisho kwa Argentina kuchukua ubingwa wa michuano ya Copa ni mwaka 1993 wakiwafunga Mexico  Magoli 2-1.

Magoli ya Argentina katika mchezo huo, magoli ya Argentina yalifungwa na Gabrile ‘Batigol’  Batistuta magoli mawili huku goli la kufutia machozi kwa upande wa Mexico likifungwa na Benjanmin Galindo.

Endapo Argentina watachukua ubingwa wa michuano ya Copa Amerika mwaka huu watafikia rekodi ya Uruguay ya kuchukua ubingwa wa michuano hii mara 15.

Timu za Argentina na Chile zimekutana mara 85 katika mashindano yote na Argentina imeshinda mara 57, mara 22 zikienda sare na Chile ikishinda mara 8 tu.

Mara ya mwisho timu hizi zimekutana katia hatua ya kufuzu katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2012 nchini Brazil.
Katika mchezo huo,Argentina walishinda magoli 2-1 kwa magoli ya Lionel Messi na Gonzalo Higuain.

Zipo takwimu nyingi zinazohusu timu hizi za Chile na Argentina katika mashindano haya ya Copa Amerika mwaka huu.

Chile ndiyo timu iliyofunga magoli mengi katika michuano hii ya Copa Amerika zaidi ya Argentina.Chile imefunga magoli 13 mpaka sasa huku Argentina wakifunga magoli 10 pekee.

Wakati Chile wakiongoza kwa kufunga magoli mengi katika michuano ya Copa Amerika,timu hiyo pia ndiyo iliyoruhusu magoli mengi  ya kufungwa kuliko timu ya taifa ya Argentina.

Chile wamefungwa magoli 4 katika michuano hiyo tofauti na magoli 3 waliyofungwa Argentina katika michuano hiyo.
Timu zote mbili zimefungana katika kucheza michezo 3 

pasipo kuruhusu goli kwa makipa Claudio Bravo wa Chile na Sergio Romeo wa Argentina.

Lionel Messi ndiye mchezaji anayeongoza kwa kupiga mashuti mengi golini akiwa amepiga mashuti 17 akifuatiwa na EDUARDO Vargas na Arturo Vidal Pado wa Chile  wenye mashuti 14 yaliyolenga goli kila mmoja.

Messi pia anashikilia rekodi ya kupiga  pasi nyingi za magoli pamoja na kiungo wa chile Jorge Valvidia wakipiga pasi 3 kila mmoja.

Hii itakuwa ni fainali ya pili kwa Argentina na Chile kukutana kwani tayari walikwishakutana mwaka 1955 na Argentina kushinda mchezo huo.Je,tutegemee Chile kulipa kisasi kwa Argentina?



0 comments:

Post a Comment