Usajili wa wachezaji kwa hatua ya
kwanza msimu huu (2015/2016) unaanza Juni 15 hadi Agosti 6 mwaka huu wakati
kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa mikataba ni kuanzia
Juni 15-30 mwaka huu.
Kipindi cha kwanza cha uhamisho wa
wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai 30 mwaka huu. Kupitia majina
na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 7 na 14 mwaka huu. Kuthibitisha
usajili hatua ya awali ni Agosti 15 hadi 19 mwaka huu.
Usajili hatua ya pili utakuwa kati
ya Agosti 17 na Septemba 8 mwaka huu. Kupitia na kutangaza majina ya pingamizi
hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Septemba 8 hadi 14 mwaka huu. Uthibitisho
wa usajili hatua ya pili ni Septemba 15 na 17 mwaka huu.
Wachezaji wanaotoka nje ya Tanzania,
usajili wa mtandao wa FIFA wa TMS utakuwa wazi kuanzia Juni 15 hadi
Septemba 6 mwaka huu. Klabu zinazosajili wachezaji kutoka nje zinatakiwa
kufanya hivyo kupitia akaunti zao za mtandao wa TMS.
Kwa klabu ambazo hazina akaunti ya
TMS zinatakiwa kuwasiliana na TFF ili mameneja wao wa usajili wapatiwe mafunzo
ya TMS, na baadaye kuombewa akaunti hizo FIFA.
Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 22 mwaka huu, na ratiba inatarajiwa kutoka
mwezi mmoja kabla (Julai 22 mwaka huu).
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inatarajiwa
kuanza Septemba 12 mwaka huu, wakati Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajia
kuanza Oktoba 17 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment