Katika michuano hiyo Ilala imetawazwa kuwa mabingwa wapya baada ya kuikandamiza mabao 3-2 timuya Alliance,katika mchezo wa fainali,huku kikosi cha Kinondoni kikimaliza katika nafasi ya tatu.
Matokeo hayo yamepigiwa makofi na uongozi wa DRFA,na kuzitaka timu hizo ziendee kukaza kamba ili kufikia mafanikio yanayohitajika katika medani ya soka
hapa nchini.
Mwenyekiti wa chama hicho,Almas Kasongo,amesema uwezo uliooneshwa na timu hizo zilizopo katika himaya yake kwa muda wote wa mashindano,zinatoa taswira za kuwapata wachezaji wazuri wa baadaye kwenye vilabu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam na kwamba ni dira ya mkoa huo kuwa kitovu cha wachezaji nguli wa wakati ujao.
Aidha
Kasongo ameipongeza Tff kwa kuwepo na mashindano hayo ya ubingwa wa taifa
kwa vijana chini ya miaka 13,na kuwataka wendeleze kwa nguvu zote mipango
waliyonayo yakuibua na kukuza vipaji vya soka kwa vijana.
0 comments:
Post a Comment