Mwenyekiti wachama hicho,Almas Kasongo, amesema matokeo hayo yamewafadhaisha mno watanzania wenye uchu wa kuona timu hiyo inapata matokeo mazuri yaliyokosekana kwa kipindi kirefu.
Amesema anaamini kuwa kikosi hicho kina wachezaji wazuri na wenye uwezo lakini wamekuwa wakikosa mbinu za kufanya vizuri kwenye timu ya taifa hasa kwenye safu ya ushambuliaji,ikilinganishwa na uwezo wanaouonesha kwenye michuano ya ligi wakiwa na klabuzao.
Hata hivyo Kasongo amesema licha ya Stars kuanza vibaya katika harakati zake za kuwania tiketi yamichuano hiyo ya afrika,bado nafasi ipo ya kujipanga upya
kwa kuanza kuangalia uwezo wa benchi la ufundi.
Aidha amesema DRFA inaamini kuwa Tff inauwezo wa kutafuta mwarobaini wa kutibu tatizo la matokeo mabaya kwa Starz,bila kumuonea mtu aibu.
0 comments:
Post a Comment