Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo imepoteza mchezo
wake wa kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa
kwa mabao 3 - 0 na wenyeji Misri.
Taifa Stars ilicheza vizuri kipindi
cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi
ya washambuliaji wa timu ya Misri, na kupelekea kwenda mapumziko -0 - 0.
Kipindi cha pili Misri walifanya
mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo 3 ndani ya dakika 10, kupitia kwa
Ramy Rabia(60), Basem Morsy(64) na Mohamed Salah (69).
Stars ilifanya mabadiliko ya
kuwaingiza Frank Domayo, Saimon Msuva na Salim Mbdonde na kufanya shambulizi
kadhaa langoni kwa Misri lakini mashambulzi hayo yaliokolewa na walinzi wa timu
ya Misri.
Mara baada ya mchezo huo, Taifa
Stars inaondoka leo Alexandria kuelekea Cairo ambapo itaondoka na shirika la
ndege la Ethiopia saa 8 usiku na kufika jijini Dar es salaam jumanne saa 7
mchana.
Tanzania: Deogratias Munish, Shomari
Kapombe, Oscar Joshua, Aggrey Morris/Salim Mbonde, Nadir Haroub, Erasto Nyoni,
Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Saimon Msuva, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata,
Amri Kiemba/Frank Domayo.
Misri: Ahmed El Shenawy, Ahmed
Hegazy, Ramy Rabea, Mohamed Abd Elshafy, Hazem Emam, Mohamed Elneny, Ibrahim
Salah, Mahmoud Abd Elmonem/Ramadan Soffiy, Mohamed Salah/Mostafa Ftahy, Doly
Elgabay/Basem Morsy, Ahmed Hassan Meky.
0 comments:
Post a Comment