Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kesho jumamosi atafunga rasmi mashindano ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13.
Sherehe ya kufunga mashindano hayo itafanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa 9 kamili alasiri .
Kwa takribani wiki moja sasa mashindano hayo yamekua
yakiendelea jijini Mwanza katika viwanja vya Alliance na CCM Kirumba.
Lengo la mashindano haya ni kuibua vipaji kwa ajili ya
kupata timu ya Taifa ya awali itakayojiandaa na fainali za vijana Afrika wenye
umri chini ya miaka 17 mwaka 2019 fainali zitafakazonyika nchini Tanzania.
Katika kutambua na kujiunga na watanzania wenzetu wenye
ulemavu wa ngozi (Albino) siku hiyo ya tareje 13/06/2015, TFF itajiunga na
familia ya walemavu wa ngozi katika kuadhimisha siku yao kimataifa na kuonyesha
bango maalum lenye kuelimisha umma juu ya ubaya wa uovu wa kuwaumiza na
kuwaua wenzetu wenye ulemavu wa ngozi.
0 comments:
Post a Comment