Main Menu

Monday, May 25, 2015

WACHEZAJI WA LIVERPOOL KUADHIMISHA MIAKA 10 YA INSTABULL



Wachezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool walioisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 2005 wameandaa sherehe kubwa ya kuukumbuka usiku wa fainali hiyo utakaoitwa ‘Muungano wa Instanbul’ itakayofanyika katika uwanja wa Echo uliopo jijini Liverpool.

Lengo la sherehe hiyo ni  kuwakutanisha wachezaji waliokuwepo katika fainali hiyo pamoja na mashabiki wake ikiwa ni miaka 10 tangu kufanyika kwa fainali hiyo.

Kutokana na uwepo wa sherehe hiyo, klabu ya Liverpool inaamini kuwa kikosi cha sasa kitajifunza mengi toka kwa wachezaji waliopita hasa nahodha wao anayeondoka Steven Gerrard.

Katika fainali ya mwaka 2005 Liverpool walicheza na klabu ya AC Milan na mpaka mapumziko AC Milan wawalikuwa mbele kwa magoli 3-0.

Kipindi cha pili Liverpool walisawazisha magoli hayo na kufanikiwa kushinda taji hilo kwa njia ya mikwaju ya penati.

Mmoja kati ya wachezaji waliokuwepo katika kikosi cha Liverpool ni mshambuliaji Djbril Cisse, Cisse anasema kuwa amekuwa akiangalia zaidi ya mara 10 penati walizopiga dhidi ya AC Milan.

Kikosi cha Liverpool kwa mwaka huo kilikuwa kikiongozwa na kocha Rafael Benitez.

Wachezaji kama Steven Gerrard,Sami Hyppia, John Arne Riise, Jamie Carragher, Milan Barros, Sanz Luis Garcia na Harry Kewell.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Ac Milan na Liverpool mwaka 2005 inatajwa kuwa ni miongoni mwa fainali bora za michuano hiyo ya Ulaya.

0 comments:

Post a Comment