Main Menu

Sunday, May 17, 2015

STARS KUANZA COSAFA KESHO NA SWAZLAND



Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kesho itashuka uwanjani katika mchezo wake wa kwanza  wa kombe la COSAFA dhidi ya Swaziland katika uwanja wa Royal Bafokeng pembeni kidogo ya jiji la Rustenburg kuanzia majira ya saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Kusini.

Uwanja wa Royal Bafokeng ni miongoni mwa viwanja viliyotumika katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika kusini, ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji  42,000 huku timu ya Platinum Stars iliyopo Ligi Kuu ya PSL ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani.

Leo jioni Taifa Stars imefanya mazoezi katika uwanja wa Royal Bafokeng kwa ajili ya kuuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe dhidi ya Swaziland.

0 comments:

Post a Comment