Main Menu

Thursday, May 21, 2015

MICHAEL VAN PRAAG AJIONDOA KUGOMBEA URAIS WA FIFA



Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Shirikisho la soka Duniani FIFA, mmoja kati ya wagombea wa kiti cha Urais Michael Van Praag ambaye pia ni Rais wa chama cha soka nchini Uholanzi amejiondoa kugombea nafasi ya Urais.

Michael Van Praag kwa sasa ana umri wa miaka 67 na alikuwa miongoni mwa wagombea watatu ambao walikuwa wakiwania kiti cha Urais wa Shirikisho la soka duniani FIFA.

Wengine ni pamoja na Prince ali Bin Ali Hussein na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno Luis Figo.

Minong’ono na tetesi za kuwa Michael hatagombea kiti cha Urais zilianza hapo jana.

Kujiondoa kwa Michael Van Praaga kunamaanisha kuwa nafasi ya wagombea wa Urais wa kiti hicho watabakia watatu ambao ni Joseph Sepp Blatter,Princ Ali Bin Hussein na Luis Figo.

Uchaguzi wa FIFA unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 29 ya mwezi huu wa tano mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment