Main Menu

Thursday, May 21, 2015

CAZORLA NDIO MPIGA PASI BORA LIGI KUU ENGLAND.



Kiungo wa klabu ya Arsenal Santi Cazorla hapo jana aliweka rekodi ya kuwa mpiga pasi bora katika Ligi Kuu ya soka nchini England na kumpita kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas katika mchezo kati ya Arsenal dhidi ya Sunderland.

Rekodi ya Cazorla inahusisha upigaji wa pasi sahihi na zilizofika katika mchezo mmoja.

Rekodi ya Cazorla hapo jana katika mchezo wa Arsenal dhidi ya Sunderland ni kupiga jumla ya pasi 155 ndani ya dakika 90.

Rekodi hii inavunja ile rekodi ya Fabregas ya kupiga pasi 144 ndani ya dakika 90 katika mchezo kati ya Chelsea na West Bromwich Albion.
Match
Accurate Pass
Mins Played
Santiago Cazorla
Arsenal vs Sunderland
155
90
Cesc Fàbregas
Chelsea vs West Brom
144
90
Cesc Fàbregas
Chelsea vs Aston Villa
133
90
Yaya Touré
Aston Villa vs Man City
128
90
Fernandinho
Sunderland vs Man City
126
90

Cazorla hakuishia hapo kwani aliweka rekodi nyingine ya kuwa mchezaji aliyegusa mpira mara nyingi kuliko mchezaji mwingine yoyote ndani ya dakika 90 za  mchezo mmoja.

Cazorla aligusa mpira mara 178 dhidi ya Sunderland na kumpita Fabregas aliyewahi kugusa mpira mara 174 katika mchezo wa Chelsea dhidi ya West Bromwich Albion.

Match
Touches
Mins Played
Santiago Cazorla
Arsenal vs Sunderland
178
90
Cesc Fàbregas
Chelsea vs West Brom
174
90
Cesc Fàbregas
Chelsea vs Aston Villa
162
90
Aaron Ramsey
Arsenal vs Sunderland
156
90

Rekodi ya mwisho ya Cazorla ni ya kupiga pasi nyingi katika theluthi ya mwisho ya timu pinzani.

Cazorla alipiga jumla ya pasi 86 ndani ya dakika 90 katika mchezo dhidi ya Sunderland, Cazorla anavunja rekodi ya David Silva aliyefanikiwa kupiga pasi 82 ndani ya dakika 90 katika eneo la mwisho la West Bromwich Albion katika mchezo kati ya Manchester City dhidi ya West Bromwich Albion.

Match
Successful Final Third Passes
Mins Played
Santiago Cazorla
Arsenal vs Sunderland
86
90
David Silva
Man City vs West Brom
82
81
Aaron Ramsey
Arsenal vs Sunderland
68
90
Cesc Fàbregas
Chelsea vs West Brom
64
90
Mesut Özil
Arsenal vs Swansea
64
90

0 comments:

Post a Comment