Main Menu

Thursday, May 21, 2015

LEONARD MCHEZAJI BORA WA ULINZI NBA



 
Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya San Antonio Spurs Kawhi Leonard amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ulinzi wa Ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani ‘NBA’.

Tuzo hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya magari ya Kia imemshuhudia Kawhi akiwashinda nyota wengine kama Draymond Green, Tony Allen na Deandre Jordan.

Katika kura za awali Draymond Green wa Timu ya Golden State Warriors alionekana kumshinda Kawhi Leonard lakini kadiri kura zilivyokuwa zikiendela kupigwa, Kawhi aliweza kupata jumla ya kura 242 huku mpinzani wake Draymond Green akipata kura 229 tu.

Tuzo za mchezaji bora wa Ulinzi katika NBA hutolewa na chama cha waandishi wa Habari za mpira wa kikapu nchini Marekani kwa kuwapigia kura wachezaji waliopendekezwa katika idara hiyo ya ulinzi.

Utoaji wa tuzo hiyo uliambatana na upangwaji wa vikosi viwili vya idara ya ulinzi.

Kikosi cha kwanza kilikuwa na nyota waliopata alama za juu katika upigaji kura wa mlinzi bora na kikosi cha pili kilihusisha wachezaji walioshika nafasi nyingine kwa mujibu wa kura za waandishi.
 Tristan Thompson dunks  Al Horford as guard Dennis Schroder  looks on  the Eastern Conference Finals
Kikosi cha kwanza kinamjumuisho wa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa ulinzi Kahi Leonard toka San Antonio Spurs, Deandre Jordan( LA Clippers),Tony Allen (Memphis),Chris Paul ( LA Clppers) na Draymond Green (Golden State Warriors).

Kikosi cha pili kina nyota kama Anthony Davis (New Orleans Pelicans),Jimmy Butler (Chicago Bulls),Andrew Bogut (Golden State Warriors),John Wall (Washington Wizards) n a Tim Duncan ( San Antonio Spurs).

0 comments:

Post a Comment