Main Menu

Friday, September 26, 2014

DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP KUANZA LEO




Makamu wa Rais wa zamani wa shirikisho la soka nchini TFF na mjumbe wa kamati ya rufaa ya shirikisho la soka barani Afrika CAF Athumani Nyamlani ndiye atakayefungua mashindano ya DR. MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP 2014.

Mashindano hayo yanayoshirikisha timu 32 yanaanza kwa mchezo wa ufunguzi kati ya timu ya Friends Rangers dhidi ya Kiluvya United katika uwanja wa mwalim nyerere makulumla magomeni.

Mchezo huo utaambatana na matukio mbalimbali ikiwemo burudani ya muziki wa kizazi kipya ambapo Makomandoo, Msaga Sumu na Mataluma wataburudisha kuanzia saa saba mchana.

Mashindano hayo yanaletwa kwa udhamini wa  Dr Mwaka ambaye ni mtaalam wa masuala ya afya ya uzazi kutoka kituo cha Foreplan clinic kilichopo Ilala Bungoni Dar  es salaam, Clouds fm na Clouds tv.

Tunasema heshima ya soka la mtaani imerudi…..
 

0 comments:

Post a Comment