Msafara wa watu 27
wa kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinaondoka kesho (Julai 30 mwaka huu)
saa 10 jioni kwa ndege ya Air Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kitapiga
kambi ya siku mbili kabla ya kuingia Maputo kuikabili Msumbiji (Mambas).
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili saa 9 asubuhi kesho
(Julai 30 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet, na baadaye jioni kuunganisha safari
ya Afrika Kusini.
Mechi hiyo ya
marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itachezwa
Agosti 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa uliopo Zimpeto nje kidogo ya Jiji la Maputo.
Msafara huo wa
Taifa Stars kwenda Afrika Kusini unajumuisha wachezaji 19 na waliobaki ni maofisa
wa Benchi la Ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij kutoka Uholanzi.
Wakati kiungo
Mwinyi Kazimoto ametua leo nchini kuungana na wenzake, washambuliaji Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu wao wataungana na wenzao kesho jijini Johannesburg
wakitokea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
***********************
SERENGETI BOYS YAWASILI SALAMA SOUTH
Timu ya taifa ya
vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 Serengeti Boys imewasili salama jana jijini
Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana
wenye umri chini ya miaka 17 dhidi Afrika Kusini (Amajimbos).
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa
za Afrika Kusini.
Timu
hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Serengeti Boys inahitaji ushindi
kwenye mechi hiyo au aina yoyote ya sare ya mabao ili ifuzu kwa raundi ya tatu.
0 comments:
Post a Comment