Main Menu

Thursday, July 31, 2014

TAIFA STARS KUJINOA SOUTH KABLA YA KUELEKEA MAPUTO MSUMBIJI



Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimewasili salama jana Mjini Johannesburg kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo, Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi mara mbili leo asubuhi na jioni kwenye uwanja wa Bed ford view Country Club.

Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho asubuhi kabla ya jioni kuanza safari kuelekea Maputo.

Wakati huo huo, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Razia Msuya leo jioni amezitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo Johannesburg kusalimia wachezaji.

Serengeti Boys yenyewe ipo Mjini humo tangu Julai 27 kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa Agosti 2 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment