Main Menu

Wednesday, January 22, 2014

YANAYOIKUMBA MBEYA NA UWANJA WA SOKOINE NILITEGEMEA

 Uwanja wa sokoine katika matengenezo
 Watoto wakiwa katika shughuli za kupanda nyasi uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Mbeya
Uwanja wa sokoine ukiwa umekamilika kwa ajili ya mashindano.


Shirikisho la soka nchini Tff imezuia kutumika kwa uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kwa michezo ya ligi kuu tanzania bara kwa klabu ya Prison iliyokua ifanyike kuanzia tarehe 25 Jan kutokana na uwanja huo kutokua katika hali nzuri.

Maendeleo ya marekebisho ya uwanja huo yalinipa mashaka toka awali pamoja na kurekebishwa kwa kiwango cha chini ili kuiwahi raundi ya pili ya ligi kuu Tanzania bara inayoanza jumamosi ya tarehe 25 January.

Pamoja na zuio la Tff naamini chama cha soka mkoa wa Mbeya kitajitahidi uwanja uwe katika hali nzuri na kuanza haraka kutumika kwa michezo ya ligi kuu ambayo imekua chanzo kikubwa cha mapato kwa chama hicho.

mechi za raundi ya 14 na 15 zinazoihusu timu ya Tanzania Prisons zilizokuwa zichezwe Januari 25 na 29 mwaka huu ndizo zilizosogewzwa mbele.

Awali Tanzania Prisons ilitakiwa kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mechi hizo dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kutokuwa tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom wikiendi hii.

Mechi hizo sasa zitachezwa kati ya Februari 6 na 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Sokoine.

0 comments:

Post a Comment